Wednesday, September 7, 2011

Thathimini ya Mfunzo ya MISA

Kwanza kabisa pole na kazi ya ujenzi wa Taifa hususani kwetu sisi Waaandishi ambao  bado hali ya Ufahamu juu ya Matumizizi ya Mtandao yanaleta shida, lakini ni kuondoe wasiwasi kwa sasa  kwani hali hiyo imebadilika tangu Tarehe 5 Sept, ni hivi karibuni tu.
Sikupi sifa ila unastahili kupewa haki inayostahili na hizi ni sifa tele kutoka kwangu, kutokana na Taaluma uliyonayo na kuamua kuitumikia na kusaidia Taifa, Wengi wanamaswali kichwani nini hasa Ambacho umefanya ila Waandishi wa  mikoa Miwili hawatokusahau kwa kile ulichokitoa tangu Tarehe 5 sept ndani ya makao makuu ya Dodoma ikiwa waandishi mkoani hapo ndio hasa tulikuwa wenyeji, na Wenzangu Wa mkoa wa Singida kule kunapopatikana hasa chakula cha asili zaidi.

Amini ufundishaji kwa watu wazima unahitaji hekima kubwa na wewe ulikuwa nayo lakini wapi palipo na kizuri kusiwe na changamoto? la hasha naimani hakuna, kama ndivyo Lazima ni bainishe kile ambacho ni Tathimini yangu ya MISA kwa ujumla.
1.Ufundishaji ulikuwa mzuri na ushirika ulikuwa wa matumaini makubwa ikiaminika uelewa ulikuwepo.
2.Bado hali ni tete katika upatikanaji wa mtandao katiak eneo lililopangwa hivyo ni vema MISA, iangalie zaidi maeneo yenye mtandao wa kutosha.
3.Siku za semina ziongezwe ili kupitia maeneo mengi zaidi
4.Kuwepo na vyeti vinavyotunukiwa.
Kwa ujumla Semina ni nzuri na Imani yangu italeta mabdiliko katika makampuni tuliyopo na jamii kwa ujumla.
Ahsante, na ninaimani hii leo upo ndani ya Iringa Ukitoka huku kwetu
Zamzam

HABARI ZENU WANA MEMBER

Mamboz

Uandishi wa kiraia na matumizi ya internet

Kipekee napenda kumshukuru Mungu kwa kunipatia nafasi hii kushiriki mafunzo haya nyeti kabisa katika maisha na utendaji wangu wa kazi wa kila siku.
 
Jambo la pili, pia niishukuru sana MISA TAN kwa kushirikiana na Shirika la masuala ya habari, mawasiliano na maendeleo la nchini Finland, VIKES, kwa kunipatia upendeleo huu kati ya wanahabari kutoka mkoa Singida, kushiriki mafunzo haya ya siku tatu, ni bahati sana.
 
Kwa kweli mafunzo haya niliyatamani kwa muda mrefu kuyapata na mara nyingi nilikuwa nikifikiri ni lini nitayapata, lakini sikuwa na jinsi; hata nilipofahamishwa kuwa nitakuwa mmoja wa washiriki huko Dodoma, nilifurahi sana.
 
Maneno yanayoandikika kwa upande wowote kama vile ADABRAKADABRA,maana halisi ya PARLE na PARLIAMENT(asili Kifaransa),nayo yalikuwa kivutio na kichekesho, yakimfanya mshiriki asiweze kuchoka na kumpa hamu na umakini wa kumsikiliza mwalimu wake. 
 
Nimejifunza mengi, hasa jinsi ya kutumia na matumizi ya blog, picha na hata habari zenyewe, na ninaamini kwa elimu hii niliyoipata itanisaidia sana katika kuboresha utendaji kazi wangu wa uandishi kwa kila siku, mkoani Singida.
 
Pia, ninamshukuru mwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Maggid Mjengwa kwa umahiri wake wa ufundishaji na kuelekeza mada alizotakiwa na MISA TAN kuwaekeleza wanafunzi wake;Mungu azidi kumtia nguvu ili siku nyingine akipata tena kibarua kama hiki,aboreshe zaidi.
 
Pamoja na mapungufu madogomadogo yaliyojitokeza mfano katika siku za kwanza upande wa mgahawa tuliokuwa tunautumia katika kulinda afya zetu, taratibu zilitoweka siku zilizofuata na hatimaye mambo yakwa mazuri; halikadhalika upande wa ukumbi na wataalamu wake(yaani UCC), kutokana na hitilafu ndogondogo,pia tunashukuru tumemaliza vizuri.
 
Mwisho kwa kadri ya uwezo wangu nitajitahidi kuitumia elimu hii niliyoipata inayoonekana ndogo machoni,lakini kwangu naiona kubwa kuweza kuitumikia jamii ya mkoa wa Singida, huku nikizingatia K3, KUJITAMBUA, KUJIAMINI na KUTHUBUTU!.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi,
 Elisante John, Singida. 

test

test2 soma zaidi; mwananchi.co.tz

mavazi kwa wanawake

Soma zaidi,mjengwa.blogspot.com

Mwenyeki na uvuvi

Mwenyekiti wa kijiji cha Mtera akivua samaki kwa ndoano; Picha zaidi mjengwa.blogspot.com

Mzee wa vijisenti akitunga sheria

mjengwa.blogspot.com/

 Ni yuleyule mzee wa vijisenti
Chenge akitafakari baada ya vijisenti vyake kufichuliwa

mjengwa.blogspot.com