Wednesday, September 7, 2011

Thathimini ya Mfunzo ya MISA

Kwanza kabisa pole na kazi ya ujenzi wa Taifa hususani kwetu sisi Waaandishi ambao  bado hali ya Ufahamu juu ya Matumizizi ya Mtandao yanaleta shida, lakini ni kuondoe wasiwasi kwa sasa  kwani hali hiyo imebadilika tangu Tarehe 5 Sept, ni hivi karibuni tu.
Sikupi sifa ila unastahili kupewa haki inayostahili na hizi ni sifa tele kutoka kwangu, kutokana na Taaluma uliyonayo na kuamua kuitumikia na kusaidia Taifa, Wengi wanamaswali kichwani nini hasa Ambacho umefanya ila Waandishi wa  mikoa Miwili hawatokusahau kwa kile ulichokitoa tangu Tarehe 5 sept ndani ya makao makuu ya Dodoma ikiwa waandishi mkoani hapo ndio hasa tulikuwa wenyeji, na Wenzangu Wa mkoa wa Singida kule kunapopatikana hasa chakula cha asili zaidi.

Amini ufundishaji kwa watu wazima unahitaji hekima kubwa na wewe ulikuwa nayo lakini wapi palipo na kizuri kusiwe na changamoto? la hasha naimani hakuna, kama ndivyo Lazima ni bainishe kile ambacho ni Tathimini yangu ya MISA kwa ujumla.
1.Ufundishaji ulikuwa mzuri na ushirika ulikuwa wa matumaini makubwa ikiaminika uelewa ulikuwepo.
2.Bado hali ni tete katika upatikanaji wa mtandao katiak eneo lililopangwa hivyo ni vema MISA, iangalie zaidi maeneo yenye mtandao wa kutosha.
3.Siku za semina ziongezwe ili kupitia maeneo mengi zaidi
4.Kuwepo na vyeti vinavyotunukiwa.
Kwa ujumla Semina ni nzuri na Imani yangu italeta mabdiliko katika makampuni tuliyopo na jamii kwa ujumla.
Ahsante, na ninaimani hii leo upo ndani ya Iringa Ukitoka huku kwetu
Zamzam

No comments:

Post a Comment